Thursday, April 6, 2017

YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA LEO


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama awasilisha nakala za matoleo ya magazeti zilizochapishwa tangu kikao kilichopita January 2017.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya  Katiba na Sheria awasilisha taarifa kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2016/2017   pamoja na maoni ya Kamati kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2017/2018.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi awasilisha taatifa ya Kamati kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ( Tume ya Uratibu na  Udhibiti UKIMWI)  kwa mwaka wa fedha 2016/2018 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu  makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2017/2018.

 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imetenga Sh Billioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja ya Shaurimoyo,  Nakalolo na Miesi.

Tutaondoa kero za tozo katika mazao. Mhe. Ole Nasha.

 Tutashirikiana na wananchi kufanya utafiti na kutenga Bajeti kwa ajili ya kituo cha utafiti Maluku. Mhe. Ole Nasha.

 Tozo zote za Bandari huzingatia uzito au ujazo wa shehena kwa mujibu wa kitabu cha Tozo za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA). Mhe. Ngonyani.

Viwango vya tozo vilivyopo katika Bandari zetu vimelenga katika kuwasaidia wafanyabiashara kupata huduma bora. Mhe Ngonyani.

Nia ya Serikali ni njema na inawawekea wafanyabiashara mazingira mazuri ya kufanya biashara zao kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za utoaji wa Huduma za Bandari. Mhe Ngonyani.