Friday, April 7, 2017
KILONGOZI ALISEMA NINI KUHUSU BODI YA MAZIWA?
Bodi ya Maziwa inajukumu la kusimamia, kuratibu na kuendeleza Tasnia ya Maziwa nchini.
Katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi, Maziwa yanachangia asilimia 18 ya pato la taifa.
Asilimia 34 ya watoto chini ya miaka mitano nchini wamekumbwa na udumavu kutokana na kutokunywa maziwa.
Tumekuwa tukifanya ushawishi kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuongeza vituo vya uzalishaji wa maziwa.
Bodi ya Maziwa huazimisha siku unywaji maziwa kwa lengo la kuhamasisha wananchi kunywa maziwa kwa kujenga afya na kukuza uchumi wa nchi.
Maziwa ni muhimu si tu katika afya ya binadamu bali pia katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuwa na wananchi wenye nguvu za kulitumikia taifa.
Afya bora ni suala muhimu katika maisha ya binadamu hasa ukizingatia unywaji wa maziwa.
Bodi ya Maziwa imelenga katika kuzalisha maziwa katika kiwango cha kimataifa.
Wananchi wanapaswa kunywa maziwa kwani huondoa udumavu na pia hupunguza vifo kwa jamii.
Bodi ya Maziwa inatarajia kuadhimisha siku ya Unywaji Maziwa Mkoani Kagera itakayofanyika Juni 1, yenye kauli mbiu isemayo *"Kunywa Maziwa Furahia Maisha"*