Wednesday, April 19, 2017
MAJIBU YA HOJA MBALIMBALI KATIKA KIKAO CHA TISA CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 19/04/2017
Serikali imechukua hatua mahsusi katika kukabiliana na changamoto zitokananazo na Agenda ya mabadiliko ya Umoja wa Ulaya-Mhe.Kolimba
Katika mwaka wa fedha 2016/17 NHC ilitenga shilingi bilioni 11 na kufanyia ukarabati nyumba 2451 katika bajeti hiyo-Mhe.Mabula
Serikali ilihakiki madai ya waliokuwa wafanyakazi wa hoteli ya 77 na kulipa shilingi bilioni 273,816,703 kugharimia mapunjo ya mishahara na mafao ya wafanyakazi hao.-Mhe.Kijaji
Wizara yangu itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutekeleza sera ya uhifadhi shirikishi ili kuboresha uhifadhi na kudumisha mahusiano na mashirikiano kati ya wahifadhi na wananchi-Mhe.Makani
Serikali imechukua hatua za kutatua changamoto ya maji katika eneo la mikumi ambapo wizara ya maji na umwagiliaji chini ya programu ya maendeleo ya sekta ya maji inatekeleza ujenzi wa mradi wa mpya wa maji wenye thamani ya milioni 809-Mhe.Kamwelwe.
Ujenzi wa barabara ya kisarawe-Maneromango mpaka sasa kilomita 7 zimeshsjengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi anaendelea na ujenzi wa kipande kingine cha mita 800.-Mhe.Ngonyani
TPA imeingia mkataba na TANROADS kwa ajili ya kuandaa ramani zitakazotoa taarifa za kijiografia kwa bandari na magati katika mwambao wote wa bahari na maziwa makuu-Mhe.Ngonyani
Serikali inategemea kuanzisha Wakala wa Maji nchini-Mhe.Lwenge