Friday, April 7, 2017

SERIKALI WILAYANI HANDENI YAPIGA MARUFUKU UKATAJI MITI OVYO

Halmashauri ya Wilaya ya Handeni waaswa kupanda miti kama zao la biashara ili kujikwamua kiuchumi badala ya kutegemea uchomaji wa mikaa uliokithiri na uvunaji mbao hali inayopelekea uharibifu wa mazingira na ukosekanaji wa mvua ya kutosha.

Rai hiyo imetolewa wakati wa kilele cha maadhimisho ya upandaji miti kilichofanyika Kiwilaya Kijiji cha kwamgunga Kata ya Kwankonje  na kueleza kuwa Serikali ilamua kuanzisha zoezi la upandaji miti baada ya kuona uharibifu mkubwa hali ambayo ingepelekea maeneo mengi kuwa jangwa.

Akizungumza kwenye zoezi hilo Katibu Tawala Wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, alisema kuwa Kwa wilaya yetu ya Handeni imeharibiwa sana na ukataji miti ambayo imekatwa kwa uvunaji mikaa, mbao na shughuli nyingine kama kuni. Mmejisahau mnakata miti bila kupanda miti matokeo yake kunabaki na jangwa ambalo linasababisha hata ukosekanaji wa mvua kwenye maeneo yetu kwa kiasi kikubwa.

Aidha aliweleza wananchi kuwa ni wajibu weo kupanda miti ili iendelee kututunza, wapande miti kama biashara kama maeneo mengine wanavyofanya hasa miti ya Mikaratusi, tafuteni maeneo mpande miti ambayo baada ya muda unavuna na inakuwa biashara kwenu itakayosaidia kuwainua kiuchumi.

”Naomba kila mmoja wetu awe ni sehemu ya kupanda miti maana nimeambiwa kijiji hiki ndio kinaongoza kwa kukata miti, viongozi wote ngazi ya Tarafa, mpaka Vijiji hakikisheni miti inapandwa na ikiwezekana kila kaya”Alisema.

Alipiga marufuku ukataji miti holela bila kupata kibali maalumu na kuwataka Viongozi kuhakikisha  wanasimamia hilo. Kila mmoja apate muamko wa kuandaa vitalu vya miti na awe na wazo la kupanda miti. Tengeni maeneo ya kupanda miti ambayo itakuwa inavunwa kama kuni badala ya kuharibu misitu. “Tuache tabia ya kuchoma moto misitu na tuache uoto wa asili kuota ili kupata miti mingine baada ya uvunaji wa miti” alisema.


Naye mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe  alisema kuwa wamekuja kupanda miti na ni jukumu la sisi wote kwa maana tunapopata upungufu wa mvua,uwepo jangwa unaathiri watu wote, wakati mwingine tunakosa hata maji ya kunywa sababu ya ukosefu wa mvua, sasa waone umuhimu wa kupanda miti kuanzia kwenye kaya zetu na kila mmoja aone kwamba anawajibu katika utunzaji wa miti .

Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepanda miche ya miti 6500 na mikorosho 800 ambapo
TFS (Tanzania Forest Service) wameweza kuchangia miche 4000.

Katibu Tawala Bw.John Mahali akipanda mti.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni Mh Ramadhan Diliwa akipanda mti.

Mkurugenzi mtendaji Be William Makufwe akifukia shimo la mche

Akinamama wakipanda miti