Tuesday, April 11, 2017
YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA TANO CHA MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 11/04/2017 MJINI DODOMA
Serikali imepanga kutumia shilingi milioni 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la upasuaji kata ya koryo,Rorya katika mwaka wa.fedha 2017/18.-Mhe.Jafo
Uamuzi wa kuifanya kata ya kyerwa kuwa makao makuu ya wilaya ya kyerwa ulitolewa baada ya kupitishwa na baraza la madiwani na kamati ya ushauri ya mkoa wa .kagera-Mhe.Jafo
kituo cha afya cha karatu kupandishwa hadhi kuwa hospitali yameanza kupitia Baraza la Madiwani.kamati ya ushauri ya wilaya na mkoa-Mhe.Jafo
Wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji imeandaa rasimu ya muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizi na udhibiti wa biashara ya chuma chakavu-Mhe.Mwijage
Serikali imeanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha mkoa wa Singida-Mhe.Ngonyani.
Ujenzi wa mradi wa maji mufindi utakaohudumia vijiji vya Sawala,Mtwango,Lufuna na Kibao unatarajiwa kukamilika 01 Juni 2017-Mhe.Kamwelwe
Mradi wa umwagiliaji wa Kitere na ile iliyopo katika bonde la mto Ruvuma tayari imekwisha ingizwa katika Mpango wa Taifa wa umwagiliaji wa mwaka 2002 ambao unafanyiwa mapitio ili uendane na hali halisi ya sasa.-Mhe.Kamwelwe
Tanzania itaendelea kutimiza wajibu wake wa kuzisaidia nchi zenye migogoro ili kuleta amani ikiombwa kufanya ivyo kwani ushiriki wetu umeleta heshima kubwa duniani-Mhe.Mwinyi
Serikali inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya tumbaku haraka iwezekanavyo-Mhe.William ole Nasha