Tuesday, April 25, 2017

YALIYOJIRI LEO BUNGENI TAREHE 25/04/2017



#Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Unakamilisha taratibu za kuwekeza kwenye vifaa tiba vitokanavyo na pamba na bidhaa za maji ya dripu-Mhe.Kaijage

#Sera ya Maendeleo ya Michezo inahimiza kila Taasisi yenye kiwanja au viwanja vya michezo kuvitunza vizuri viwanja hivyo ili viweze kudumu-Mhe.Wambura

#Halmshauri kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Biharamulo imewezesha jumla ya waendesha bodaboda 410 kupata mafunzo ya uendeshaji wa pikipiki na kuwapatia leseni.-Mhe.Jafo

#Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeziagiza Halmashauri  zote nchini kuainisha maeneo yanayoweza kujengwa Mabwawa na kutenga fedha kwenye bajeti zao za kujenga angalau bwawa moja kila mwaka-Mhe.Kamwelwe

#Serikali imeandaa mkakati wa kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwa ambayo hupelekea ajali za barabarani kuongezeka-Mhe.Mhe.Masauni

#Matawi ya Shirika la Taifa la Usagishaji(NMC) yaliyobinafsishwa ni 22 na yaliyobaki mikononi mwa Serikali ni matano,katika ubinafsishaji huo Serikali imepata shilingi bilioni 7,491,611,000.

#Kwa mujibu wa Sheria Serikali hairuhusu usafirishaji wa mbao zenye unene wa sentimeta 20-Mhe.Makani

#Imethibitika kwamba kilimo cha kuhamahama ikiwa ni pamoja na utumiaji wa maeneo makubwa ya ardhi,ufugaji wa kuhamahama ukijumuisha uingizaji wa mifugo katika maeneo yaliyohifadhiwa ni matumizi mabaya ya rasilimali ardhi yasiyo na tija kwa taifa-Mhe.Makani

#Hadi sasa shilingi bilioni 1.9 zimetumika kwa ajili ya kuunganisha maji kwa vijiji 13 kutoka bomba kuu la ziwa Victoria-Mhe.Ngonyani

#Ujenzi wa kiwango cha lami wa  barabara ya Kasulu-Manyovu unatarajiwa kuanza baada ya kukamilika kwa mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.-Mhe.Ngonyani

*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*