Mhe:Seleman Jafo akihutubia katika kikao kazi cha maafisa habari jijini Arusha hivi karibuni |
Mhe:Harrison Mwakyembe katika ufunguzi wa kikao cha Maafisa habari hivi karibuni jijini Arusha(picha na Mlyambate Blog) |
Mhe Mwakyembe akisalimiana na watendaji wa wizara ya habari(picha na Mlyambate Blog) |
Maafisa habari katika utaaali wa ndani wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Tarangire |
Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo katika kikao cha maafisa habari Jijini Arusha |
Maagizo hayo ameyatoa hivi karibuni katika hitimisho la kikao cha 14 cha maafisa habari wa serikali kilichofanyika jijini Arusha,amewataka maafisa habari hususan wa mamlaka za serikali za mitaa kuwa makini na weledi wa shughuli na miradi inayotekelezwa na serikali na kuwajuza wananchi hatua kwa hatua.
Mhe.Jafo amewataka maafisa habari kujiamini katika kuisemea serikali na kuhakikisha wanakuwa na vitendea kazi kama kamera na kompyuta ili kuzifanya kazi zao katika ubora na kwa afisa habari asiyetaka kufanya kazi yake serikali haitakuwa na nafasi na mtu wa aina hiyo.
Aidha Waziri Jafo ameziagiza taasisi za serikali kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi kwa maafisa habari wa taasisi na mamlaka za serikali za mitaaili kazi ya kuisemea serikali ifanyike kwa tija na kusiwepo kisingizio cha kutofanya kazi kwa kutokuwa na vitendea kazi.
Katika hotuba yake ya ufungaji wa kikao kazi hicho aliagiza wakuu wa idara wa halmashauri nchini kutoa takwimu sahihi kwa maafisa habari zinazohusiu miradi mbalimbali na kutoa ushirikiano wa hali ya juu bila kuchelewa ili wasemaji hawa wa taasisi wafanye kazi zao kwa wakati.
Jafo alimalizia hotuba yake kwa kuwaagiza wakuu wa taasisi kuwaruhusu maafisa habari washiriki vikao vyote vya maamuzi katika halmashauri na taasisi zingine ili wafahamu masuala yote yanayofanyika katika taasisi za serikali ili wawe na uhakika na kujiamini kwa kile wanachojuza umma wa watanzania.