Wednesday, March 29, 2017

MAJINA YA WAGOMBEA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI YATANGAZWA







Kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi imekutana leo  katika ofisi Ndogo ya Chama cha Mapinduzi Jijini Dar as salaam chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuteua wagombea na kutangaza wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye mkutano wa Bunge mwezi ujao.
Akisoma majina hayo leo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Pole pole amesema kuwa wameteua wananchama hao miongoni mwa wanachama zaidi ya 450 waliokuwa wamechukua fomu kugombea nafasi hizo.
Aidha, amesema kuwa wabunge 9 watakaokwenda kwenye Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6 watatoka CCM. ambapo ameongeza kuwa wanne watatoka Tanzania Bara na wawili watatoka Zanzibar.
Majina aliyoyataja Polepole, ni pamoja na  Zainabu Kawawa, Happines Lugiko, Fancy Nkhuhi, Happines Mgalula, Dkt Ngwaru Maghembe, Adam Kimbisa, Anamringi Macha na Makongoro Nyerere.
Kwa upande wa Zanzibar majina yaliyopitishwa kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki ni pamoja na Maryam Yahya, Rabia Hamid, Abdallah Makame na Mohammed Nuh.
Hata hivyo, Pole pole amesema kuwa miongoni wa wagombea hao 12, Bunge litapiga kura kuchagua wabunge sita ambapo watatu ni wa kike, na wengine watatu wakiume watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi,Humphrey Polepole.