Friday, March 31, 2017

YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA NCHINI TANZANIA LEO TAREHE 31/03/2017



#ZiarayaWaziriMkuuEthiopia:Serikali ya Tanzania na Ethiopia imesaini mikataba mitatu.

#ZiarayaWaziriMkuuEthiopia:Mkataba wa kwanza unahusu Mkakati wa Ushirikiano Kati ya Serikali ya Tanzania na Ethiopia.

#ZiarayaWaziriMkuuEthiopia:Lengo la mkataba wa kwanza ni kupambana na tatizo la uhamiaji haramu, ushirikiano kwenye masuala ya biashara,uwekezaji,teknolojia na afya.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia:Mkataba wa pili unahusu Kuanzisha Kamisheni ya Pamoja ya Kudumu Kati ya Serikali ya Tanzania na Ethiopia.

#Lengo la mkataba wa pili ni kuanzisha kamati ya kudumu kati ya Wizara za Mambo ya Nje ya Nchi zote mbili kwa kushirikiana na sekta zingine katika masuala ya uchumi na jamii.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia:Mkataba wa tatu unahusu Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Utalii kati ya Serikali ya Tanzania na Ethiopia.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia:Lengo la mkataba wa tatu ni kutoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa Sekta ya Utalii.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali kutoa ushirikiano mkubwa katika sekta ya usafirishaji wa mizigo kwa ndege -Rais Magufuli.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali kufanya biashara kwa kutumia bandari yetu-Rais Magufuli.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali kutuma wataalam kwa ajili ya kujenga mabwawa ya kuzalisha umeme -Rais Magufuli.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali matumizi ya mto Nile yanufaishe nchi zote zinazozungukwa na mto huo -Rais Magufuli.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali kutoa megawati 400 kutoka katika mabwawa yao kwa ajili ya kusaidia uzalishaji wa umeme Tanzania -Rais Magufuli.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali kufungua ubalozi mkoani Dodoma-Rais Magufuli.

 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Rais Magufuli amekubali kutoa eneo kwa ajili ya kujenga makazi na ofisi ya ubalozi huo mkoani Dodoma.

 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali kuchagua Chuo Kikuu kimoja kwa ajili ya kufundisha kiswahili-Rais Magufuli.

 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Rais Magufuli.ameahidi kupeleka wataalamu wa lugha ya kiswahili ili wakafundishe chuoni hapo.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Serikali ya Ethiopia imekubali  kuleta wataalam kutoa mafunzo katika mchezo wa riadha-Rais Magufuli.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Tanzania inaweza ikawa nguzo katika maendeleo ya Kanda ya Afrika - Waziri Mkuu, Haile Mariam Dessalegn.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Tanzania ni mfano mzuri sana katika maendeleo ya kilimo- Waziri Mkuu, Haile Mariam Dessalegn.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Tanzania na Ethiopia hatushindani bali tunasaidiana-Waziri Mkuu, Haile Mariam Dessalegn.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Tanzania na Ethiopia imepitia katika historia inayofanana hivyo tunaweza tukabadilishana uzoefu utakaoleta maendeleo baina yetu- Waziri Mkuu, Haile Mariam Dessalegn.
 #ZiarayaWaziriMkuuEthiopia;Lazima tujielekeze katika kusaidia maendeleo katika ngazi ya familia- Waziri Mkuu, Haile Mariam Dessalegn.

HABARI NI UHAI WA DEMOKRASIA