Wednesday, April 5, 2017

KILICHOJIRI BUNGENI LEO



                                                  Bungeni mjini Dodoma leo
 Ujenzi wa jengo la upasuaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele lipo katika hatua za umaliziaji na limegharimu Sh Millioni 481. Mhe. Suleiman Jafo

 Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele ni miongoni mwa vipaumbele vya Wilaya. Mhe Jafo

 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imepanga kukiboresha kituo cha Afya Iyonga ili kiweze kutoa Huduma zenye hadhi ya Hospitali ya Wilaya. Mhe. Jafo

 Serikali ipo tayari kuboresha huduma za Afya katika Wilaya Mvomero Morogoro na Wilaya zingine Tanzania. Mhe. Jafo

 Ujenzi wa Chujio na Usambazaji wa maji katika Mji mdogo wa Mugumu Serengeti utakamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo mwezi June 2017. Mhe. Jafo

Mradi wa Chujio la maji katika Mji Mdogo Mugumu umegharimu sh Billioni 1.49 na utekelezaji wake umekamilika kwa asilimia 62.5. Mhe. Jafo

 Serikali imetenga Billlioni 19 kwa ajili ya kuboresha usambazaji wa maji katika Mji mdogo Mugumu Serengeti. Mhe. Lwenge

 Serikali imetenga Bil 2 kwa ajili ya kuboresha maji katika Wilaya ya Korogwe. Mhe Lwenge.

 Ujenzi wa mradi wa maji Lumeya- Kalebezo- Nyegonge ulianza kutekelezwa mwezi March 2013 kwa gharama ya Sh Billioni 1.69. Mhe. Jafo

 Mradi huu wa maji upo katika hatua za mwisho na utakamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo Juni 2017. Mhe. Jafo.

 Mradi  huu wa maji utanufaisha wakazi 16,000 wa vijiji vya Kalebezo na Nyegonge. Mhe. Jafo

Hadi sasa kuna Miradi Miwili inayosafirisha Gesi Asilia kutoka Mtwara -Lindi hadi Dar es Salaam. Mhe Kalemani

 Miradi hiyo ni pamoja na mradi mpya wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara - Lindi hadi Dar es Salaam uliokamilika mwaka 2015 na mradi wa Songas uliokamilika mwaka 2004. Mhe Kalemani

 Gesi Asilia kutoka Lindi na Mtwara inazalisha takribani asilimia 50 ya umeme unaotumika nchini. Mhe Kalemani

 Kwa sasa Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania inatekeleza Mradi wa kuunganisha gesi katika Kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara. Mhe Kalemani.

 Naipongeza Serikali kwa kupelekeka umeme kupitia mradi wa REA kwa vijiji vya Newala. Mhe  Mkuchika.

Serikali inaboresha hali ya upatikanaji wa Umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na kujenga njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 132 yenye urefu wa kilometa 80 kutoka Mtwara hadi Mnazi Mmoja Lindi. Mhe. Kalemani

 Gharama za kuunganisha umeme vijijini kupitia Mradi wa REA ni Sh 27,000. Mhe. Kalemani.

 Serikali inajenga mradi wa kusafirisha umeme wa Kilovoti 400 kwa mikoa ya Mbeya na Songwe inatarajia kupunguza tatizo la upatikanaji wa Umeme. Mhe. Kalemani.

 Tunaimarisha kwa kuimarisha usambazaji na  kuongeza kilovoti 20 katika upatikanaji wa Umeme Wilaya ya Temeke. Mhe. Kalemani

Kodi ya Kampuni inatozwa sehemu ambapo kampuni imesajiliwa yani Tanzania Bara au Zanzibar. Mhe. Kijaji

 Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya China, Benki ya Maendeleo ya Waarabu, Washirika wa Maendeleo, na mkopo kutoka katika Serikali ya India zimetoa jumla ya Sh Billoni 23.4 kwa ajili ya mradi wa maji awamu ya kwanza Chalinze: Mhe Lwenge

 Awamu ya Pili ya Mradi  wa maji Chalinze unagharimu jumla ya Sh Billioni 53.7 na  Sh Billioni 86.9 kwa awamu ya tatu. Mhe. Lwenge

 Baada ya kukamilika ka mradi Maji Chalinze awamu ya kwanza na ya pili  utanufaisha  jumla ya Vijiji 88 kwa wakazi waishio katika eneo linalopita mradi. Mhe. Lwenge

 Vijiji vya Mwindu, Visakazi, Lulenge, Tukamisasa, Kinonko, Bwawani, Sinyaulime, Gwata, Ngerengere, Kidugalo, Kambi ya Kinonko na Sangasanga ambavyo vipo katika awamu ya pili vitaanza kunufaika na mradi mwishoni wa mwezi Aprili 2017. Mhe Lwenge

 Katika kuendeleza Skimu ya Umwagiliaji ya Ikweha Mufindi, Serikali ilitekeleza mradi huo kwa awamu mbili. Mhe Lwenge

 Awamu ya kwanza ya Mradi wa umwagiliaji wa Ikweha ilitekelezwa kwa gharama ya Sh Millioni 435.9 na awamu ya pili itatekelezwa kwa gharama ya Sh Millioni  370.7. Mhe. Lwenge

 Serikali inatambua umuhimu wa kujenga mabwawa kama hatua muhimu ya kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na kuimarisha usalama wa chakula kupitia kilimo cha umwagiliaji. Mhe Lwenge.

Serikali katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018  itafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa mabwawa mbalimbali ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji nchini. Mhe Lwenge

 Serikali haijafanya Operesheni yoyote ya kuwaondoa wananchi katika maeneo ya Hifadhi ya Geita bali ipo katika mjadala unaofuata njia ya kutatua tatizo hili bila kuleta athari hasi na kubwa kwa maisha ya wananchi. Mhe. Makani