Tuesday, May 2, 2017
KAMATI YA MAADILI YA BUNGE YAWASAMEHE MAKONDA NA WENZIE
#Natoa wito kwa halmshauri zote nchini kutenga maeneo rafiki ya kufanyia biashara kwa ajili ya wafanyabiashara wadodgo wadogo,kupeleka fedha kwenye mifuko na kusimamia marejesho ili ziweze kunufaisha makundi mengine-Mhe.Jafo
#Programu ya kupanga,kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini na itahusisha Halmashauri zote nchini na imepangwa kufanyika katika kipindi cha miaka kumi katika awamu mbili za miaka.mitano kwa kila awamu kuanzia mwaka wa fedha 2016/17-Mhe.Mabula
#Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi inafanya rejea ya mfumo bora wa kuzalisha mbegu za pamba kwa maana ya kuboresha zaidi-Mhe.Ole Nasha
#Serikali imeendelea kuongeza fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hadi kufikia bilioni 8 kwa mwaka 2016/17-Mhe.Kijaji
#Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi ilielekezwa kuandaa waraka wa Baraza la Mawaziri wenye mapendekezo ya namna bora ya matumizi ya mashamba hayo.-Mhe.Kijaji
#Watu Wenye ulemavu wamezingatiwa katika makundi ya watu wanaostahili msamaha wa uchangiaji huduma za afya na msamaha huo utazingatia kama mlemavu huyo atabainika kuwa hana uwezo wa kulipia huduma-Mhe.Kigwangala
#Natoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwabaini,kuwafichua na kuwakamata ili mkondo wa sheria uchukue nafasi yake-Mhe.Masauni
*HOJA ZA KAMATI YA HAKI,MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE NA MAAMUZI YA BUNGE*
#Bunge limeamua kumsamehe Mhe.Freeman Mbowe baada ya kukiri kudharau mamlaka ya Spika.
#Kamati ya bunge pia imempa onyo kali Mhe.Ester Bulaya baada ya kukiri kudharau Mamlaka ya Bunge.
#Bunge limemsamehe Mhe.Halima Mdee lakini limempa sharti la kutotenda kosa kama hilo tena la kudharau kiti cha spika na endapo atarudia atapewa adhabu bila kupitia kamati yoyote
#kamati iyo pia imemsamehe Bw.Paul Makonda na Bw.Alexander Mnyeti kwa kosa la kuingilia Uhuru na haki za Bunge.
*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*