Mafunzo ya uandishi wa tovuti
yamezinduliwa rasmi leo katika manispaa ya Iringa kwa maafisa habari na Tehama kutoka
mikoa ya Iringa ,Njombe,Singida,na Pwani.Mafunzo hayo yamefunguliwa leo na Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano serikalini ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Rebecca Kwandu.
Katika hotuba yake ya ufunguzi aliwataka
washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini na utayari katika kujifunza kwani taaluma
ya uandishi ni taaluma kama taaluma zingine. Hivyo mafunzo haya tunataka
yakazae matunda kwa washiriki ili waweze kuisemea serikali kwa umakini kama
maagizo Waziri wa TAMISEMI Mhe Jafo alivyotoa maagizo kwenye kikao kazi cha
maafisa habari wa serikali kilichofanyika jijini Arusha hivi karibuni.Katika
mafunzo haya ya uandishi wa tovuti ni utekelezaji wa vitendo kwa maagizo ya
serikali ya kuwataka maafisa habari wawe wasemaji wa taasisi zao kwa kuujuza
umma yanayotekelezwa na serikali kupitia tovuti za halmashauri na mikoa Kwandu
alisistiza.
Kwa upande wake Mkuu wa
mawasiliano wa Shirika lisilo la kiserikali USAID/Tanzania linaloshughulikia
Uimarishaji wa mifumo ya ya Sekta za Umma(PS3) Bi Leah Mwainyekule amewataka
washiriki kujifunza kwa vitendo ili watakapomaliza mafunzo haya tovuti zikawe
hai na watanzania wakapate habari za masuala mbalimbali yanayofanywa na
serikali sanjari na elimu kwa umma kupitia tovuti.
Mafunzo haya yanafanyika muda
muafaka kwani ni siku tatu zimepita tangu kufungwa kwa kikaokazi cha maafisa
habari wa serikali pale alipoagiza Mhe Jafo maafisa habari waisemee serikali
kwani ni miradi mingi inatekelezwa na serikali ya awamu ya tano lakini wananchi
hawajui kinacho endelea. Kikao kazi hiki kitafanyika kwa siku nne na baada ya
hapa mafunzo haya yatafanyika kwa maafisa habari wa mikoa ya
Mbeya,Katavi,Songwe,Rukwa,Ruvuma,Lindi na Mtwara.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Rebecca Kwandu akifungua Mafunzo ya Maafisa Habari(aliyesimama) |