Ujenzi wa nyumba ya mganga katika kituo cha afya Lugoba wilayani Chalinze |
Ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika kituo cha afya Lugoba |
Na John Mlyambate
Kero ya ukosefu wa huduma za afya kubaki historia kwa
wananchi wa kata ya Lugoba na maeneo yanayozunguka eneo hilo,kauli hiyo
imetolewa na wakazi wa kijiji cha Lugoba hivi karibuni baada ya serikali ya
awamu ya tano kutoa fedha shilingi za kitanzania milioni 400 kwa ajili ya kujenga
miundombinu ya huduma za afya kwa maana ya maabara,jengo la upasuaji,jengo la
mama na mtoto,jengo la kuhifadhia maiti na nyumba ya mganga.
Mwanahabari wa halmashauri alipokuwa akitembelea kituo cha
afya Lugoba alikutana na wanachi waliokuwa wakipata huduma ya matibabu kituoni
hapo ndipo walipopaza sauti na kusema “Sasa Lugoba kero ya huduma za afya siyo
hoja”.Kauli hii ilitolewa na Bi Pili Haji na kushangiliwa na wagonjwa waliokuwa
mahali pale kuashiria kero imepata ufumbuzi.
Pili aliendelea kwa kueleza kuwa baada ya kukamilika kwa
majengo haya hakutakuwa na sababu ya wananchi kwenda hospitali ya wilaya
Bagamoyo au hospitali teule ya mkoa wa
Pwani Tumbi kwani mpaka sasa ikitokea mama mjamzito ameshindwa kujifungua kwa
njia ya kawaida inabidi apelekwe hospitaki ya Tumbi kitu ambacho ni hatari kwa
akina mama wajawazito.
Naye Bi Mwajabu Makame mkazi wa kijiji cha Lugoba
allishukuru serikali kwa hatua inazoendelea nazo katika kuwahakikishia wananchi
upatikanaji wa afya bora,ili kunusuru maisha ya mama na mtoto katika kata yetu
na Chalinze kwa ujumla.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri ya Chalinze Dkt.Rahim
Hangai akiwa eneo la ujenzi alifafanua kuwa,ujenzi huu wa miradi ya afya
unatarajiwa ukamilike mapema na kwa wakati kwani fedha kwa ajili ya mradi huu
ipo na inaendelea kutumika na muda si mrefu miundombinu hii itakamilika na
kuanza kutumika kama yalivyo malengo ya serikali kuhusu afya.