Thursday, April 13, 2017
*YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA SABA CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 13/04/2017 MJINI DODOMA.*
*Bunge limepokea hati mbalimbali ikiwemo*
.Ripoti ya mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali za mitaa kwa mwaka wa Fedha unaoishua tarehe 30 Juni 2016
.Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi juu ya Udhibiti wa Uendelezaji wa maeneo ya wazi yaliyo ainishwa nchini.
.Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi juu ya miundombinu ya shule za msingi Tanzania
.Taarifa ya majibu ya Serikali na Mpango kazi wa utekelezaji wa mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa hesabu za mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha ulioshia 30 juni 2016.
.Ripoti ya mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu taarifa za fedha za Serikali kuu kwa mwaka wa fedha unaoishia tar 30 juni 2016
.Ripoti ya mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu Taarifa xa fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha unaoishia tar 30 juni 2016.
.Ripoti ya mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu taarifa za fedha za mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha unaoishia tar 30 juni 2016.
.Ripoti ya jumla ya ukaguzi wa ufanisi na ukaguzi maalum kwa kipindi kinachoishia tar 30 juni 2016
.Ripoti ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi katika taarifa tano za ukaguzi wa ufanisi zilizotolewa na kusomwa Bungeni kuanzia mwaka 2012-2013.
.Majibu ya hoja na mpango wa kutekeleza mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa hesabu za Serikali kwa hesabu za Serikali kuu na Mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
.Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi juu ya uzalishaji wa wahitimu katika sekta ya mafuta na gesi asilia.
.Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi juu ya usimamizi wa samani za barabara.
.Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi juu ya usimamizi wa kaguzi za vyombo vya majini kwa ajili ya kupewa vyeti vya ubora na kukidhi viwango vya usalama wa usafirishaji.
.Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi katika usimamizi wa uchukuaji wa maji kutoka vyanzo vya maji.
.Ripoti ya ukaguzi wa ufanisi juu ya usimamizi wa mikataba iliyoingiwa kati ya Serikali na Hospitali za Binafsi nchini.
*MAJIBU YA HOJA MBALIMBALI LEO BUNGENI*
#Mwekezaji wa mradi wa mabasi ya mwendokasi hakupata msamaha wa kodi wakati wa kuingiza mabasi nchini bali alipewa punguzo la kodi-Mhe.Jafo
#Urasimishaji unatoa fursa kwa wananchi kutumia ardhi kupitia nyaraka za umiliki wa ardhi(hati) kuweka dhamana ya mikopo katika Taasisi za fedha,mahakama n.k-Mhe.Mabula
#Mkandarasi aliyejenga barabara ya Kilindoni-Utende ameelekezwa kurudia kwa gharama zake mwenyewe maeneo yote yaliyoonekana kuwa na mapungufu kulingana na matakwa ya mkataba-Mhe.Ngonyani
#Mradi wa ujenzi wa makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe utaendelea kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2017/18-Mhe.Ngonyani
#Tumeboresha miundombinu ya umeme na kuweka umeme wa msongo mpya kutoka Kv 220 mpaka Kv 440 katika mkoa wa Kilimanjaro.-Mhe.Muhongo.
*Bunge limehairishwa mpaka Jumanne tarehe 18/04/2017 kupisha sikuu za Pasaka*