Wednesday, April 12, 2017
YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA SITA CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 12/04/2017 MJINI DODOMA
Ofisi ya makamu wa Rais kukamilisha mkakati wa Taifa wa miaka mitano wa kupanda na kutunza miti utakaotumia bilioni 105.-Mhe. Mpina
Serikali inaendelea na mchakato wa ndani wa kufanyia marekebisho ya kuhuisha na kuimarisha sheria ya ndoa ya mwaka 1971.-Mhe.Kabudi.
Serikali kuendelea na mkakati wa kuendeleza sekta ya alizeti nchini.-Mhe.Mwijage
Serikali inajadili mapendekezo ya kuwa na mamlaka ya mji mdogo wa haydom-Mhe.Jafo
Serikali kupitia halmashauri imeweka utaratibu wa kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji,vitongoji na mitaa kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri-Mhe.Jafo
Nchi haina tatizo la upungufu wa dawa za ARVs kwa watoto.-Mhe.Ummy Mwalimu.
Upanuzi wa barabara ya mbeya kwenda zambia utaanza pale upembuzi yakinifu na usanifu wa kina utakapokamilika.-Mhe.Ngonyani.
Wizara ya Afya kushirikiana na TAMISEMI imeanzisha mpango wa kuimarisha ulinzi na usalama kwa watoto ambapo halmashauri 51 zimewezeshwa kuunda timu za ulinzi wa watoto.-Mhe.Ummy Mwalimu.
Serikali ina mpango wa kununua magari mapya ya zimamoto na uokoaji kwa ajili ya mikoa mbalimbali nchini-Mhe.Mwigulu.