Wednesday, March 14, 2018

Mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao cha maafisa habari wa serikali leo Jiji Arusha



*Umuhimu wa Mawasiliano ya Kimkakati Katika Kuisemea Serikali - Dkt. Hassan Abbasi.*

#Afisa Habari anatakiwa kutumia njia zote za Mawasiliano kufikisha taarifa kwa wananchi.

#Maafisa Habari tunathaminiwa na ndio mana tupo kwenye muundo wa Serikali hivyo kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii.

#Afisa Habari anatakiwa kuifahamu vizuri Taasisi yake pamoja na takwimu zote zinazohusu taasisi hiyo.

#Maafisa Habari tusisubiri taasisi zetu zisemwe ndio tuongee, tuwe na vipindi kwenye televisheni,redio na kwenye magazeti.

*Mambo Muhimu kwa Maafisa Habari kwa Mujibu wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa na Kanuni Zake - Wakili Kamana Stanley Kamana.*

#Maafisa Habari mkitimiza vyema wajibu wenu chini ya Sheria ya Haki ya kupata Taarifa, utamaduni wa uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa shughuli za taasisi zenu utaimarika na kuleta matokeo mazuri katika ustawi wa Taifa letu.

#Afisa Habari anatakiwa kuyafahamu masharti ya Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa na Kanuni zake na kuitekeleza kikamilifu.

#Afisa Habari anatakiwa kufahamu kwa kina muundo wa taasisi anayoitumikia, majukumu na aina ya taarifa zinazozalishwa na taasisi hiyo.

*Mambo Muhimu kwa Maafisa Habari Katika Sheria ya Huduma za Mwaka 2016 na Kanuni zake za Mwaka 2017 - Wakili Patrick Kipangula.*

#Afisa Habari anawajibu wa kuishauri Serikali kuhusu mawasiliano ya kimkakati katika eneo lake la kazi.

#Afisa Habari anawajibu wa kuwezesha mawasiliano ndani ya Serikali na kati ya Serikali na Umma.

#Afisa Habari ana wajibu wa kuuhabarisha Umma kuhusu masuala ya maendeleo ya Taasisi yake.

*Wajibu wa Maafisa Habari Katika Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Maafa - Harrison Chinyuka.*

#Maafisa Habari wanatakiwa kueleza Taasisi au Idara zao namna ya kujiandaa iwapo maafa yatatokea.

#Maafisa Habari wanatakiwa kutoa taarifa za mahitaji pindi maafa yanapotokea katika maeneo yao ya kazi, mfano uhitaji wa mahema.

#Jamii ijengewe uwezo wa kukabiliana na maafa hususani kwa kupata taarifa sahihi.

*Uzoefu wa Mbinu za Kupambana na Dharura (Crisis) Katika Kuisemea Serikali - Dkt. Cosmas Mwaisobwa.*

#Mawasiliano ni muhimu wakati wa mzozo (Crisis) ili Wananchi wajue nini kinaendelea.

#Taasisi inatakiwa kutumia vyombo vya habari kutoa taarifa za mara kwa mara ili Wananchi wajue tatizo linashughulikiwa.

#Kutoa ahadi za uongo hakusaidii kutatua mzozo bali kunaongeza mzozo kati ya Taasisi husika na Wananchi .

*Data Stories, Mkurugenzi Mtendaji Twaweza, Aidan Eyakuze.*

#Afisa Mawasiliano anamvusha Mwananchi kutoka kwenye giza la mkanganyiko wa sintofahamu kwenda kwenye hali ya nuru na uhakika.

#Afisa Mawasiliano ni daraja kati ya Serikali na Wananchi na Wananchi na Serikali.

#Taarifa ikiwa huru Wananchi wana imani kuwa wana haki ya kuchangia taarifa hiyo.

*Namna ya Kujiwekea Akiba na Maandalizi ya Kustaafu, Anselm Namala.*

#Kama kustaafu ni hakika, kufikiria kuhusu kustaafu ni jambo lisiloepukika.

#Maandalizi ya kustaafu yaanze siku ambayo unapata barua ya kuanza ajira.

#Asilimia 78 ya mtaji wa kuanzia biashara wakati wa kustaafu hupatikana wakati wa ajira.

*Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO.*