Tuesday, March 28, 2017

TOVUTI ZA SERIKALI HEWANI RASMI

TOVUTI ZA SERIKALI KUBORESHA USIMAMIZI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI
Sekretarieti za mikoa yote 26 ya Tanzania Bara  na Halmashauri zake 185,zimezindua tovuti zake  mpya katika uzinduzi wa  kitaifa,tukio hili limefanyika mkoani Dodoma mgeni rasmi akiwa Waziri wa  Nchi,Ofisi  ya Rais  -Tawala za mikoa na Serikali  za Mitaa,Mh George Simbachawene.Uzinduzi huu wa  kitaifa umeshirikisha mawaziri na viongozi mbalimbali wa  Serikali akiwemo Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais  Menejimenti ya utumishi wa  Umma. Angela Kairuki,Waziri wa  Habari,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe,na Mkurugenzi wa  USAID/Tanzania,Tim Donnay,pia walihudhuria.
Kwa upande wa  uzinduzi wa  tovuti kwa Kanda ya kisini ulifanywa na mkuu  wa  Wilaya ya Mtwara Mhe.Evodius Mmande kwa niaba ya Mkuu wa  mkoa  wa  Mtwara.
Katika hotuba yake  ya uzinduzi alisisitiza kwa maafisa habari  kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa  mafunzo na sheria za habari  nchini.Ikiwa ni  pamoja na kutoa habari  zilizochambuliwa na kufafanuliwa vizuri ili ujumbe uwafikie wananchi kwa wakati na zisiwe na madhara kwa wananchi.
Mhe.Mmande amewataka wakuu wa  taasisi kuondokana na urasimu wa  utoaji taarifa kwa maafisa habari  kwani utoaji taarifa kwa umma ni  suala la kisheria halihitaji urasimu.
Aidha amesema kuhusu upungufu wa  watumishi wa kada za Tehama na Habari katika halmashauri na sekretarieti za mikoa ni  changamoto inayoweza kupelekea tovuti hizi kutofanya kazi zake  ipasavyo.
Ametoa Rai kwa TAMISEMI na Utumishi kuhakikisha kada hizi zinapata watumishi kwani ni  muda muafaka kuwa na watumishi hawa.
Mwisho,mgeni rasmi aliishukuru serikali  ya Marekani kupitia shirika lake la misaada la USAID,PS3,TAMISEMI,EGA na washiriki wote  wa mafunzo na kuwataka washiriki kuyatekeleza kwa vitendo mafunzo waliyoyapata,na akazindua tovuti 26 za mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara.