Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo awataka
waajiri na wafanyakazi kuheshimu sheria za utumishi wa umma kwa kila mmoja
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za nchi,ameyasema hayo katika
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyoadhimishwa kimkoa katika
halmashauri ya Mji wa Kibaha Jana katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha na
kukemea tabia za baadhi ya waajiri wasiotaka kufuata sheria za utumishi kwa
kunyanyasa wafanyakazi hatakuwa tayari kufanya kazi na watu wa aina hiyo katika
mkoa wa Pwani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo(katikati) akiimba wimbo wa wafanyakazi |
Wafanyakazi bora wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze katika maandamano |
Wafanyakazi hodari kutoka halmashauri ya Chalinze wakiwa na furaha kwa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani |
Wafanyakazi bora wakiongozwa na afisa utumishi wa Chalinze Ruth Timba |
Wafanyakazi hodari wakiwa katika viwanja vya shirika la elimu kibaha |
Chalinze Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee |
Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee |
Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee |
Meza kuu wakati wa Mei Mosi 2018 |
Viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya mei mosi 2018 |
VIongozi mbaimbali |
Wafanyakazi hodari baada ya kutunukiwa zawadi zao |
Solidarity forever |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze,Bwana Edes Lukoa Akijitambulisha katika kusanyiko la mei mosi |
Wafanyakazi hodari wakipeana hongera |
Mkuu wa Mkoa wa Pwani akitoa hotuba yake katika siku ya Mei Mosi |
Wafanyakazi wa Chalinze ktika picha ya pamoja na Mkurugenzi wao |
Picha ya Pamoja baada ya maadhimisho |
Akisoma Risala ya shirikisho la wafanyakazi(TUCTA )Mkoani
Pwani Bwana Ramadhani Kinyagoli aliishukuru serikali kwa jitihada zake katika
shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na serikali ya awamu ya tano kwa maslahi
ya watanzania wakiwemo na wafanyakazi,hata hivyo hakusita kuwasilisha madai na
changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa mkoa wa Pwani ikiwa ni
pamoja na wafanyakazi kutopandishwa vyeo kwa wakati,kodi kubwa ya
mshahara,wastaafu kutolipwa mafao yao kwa wakati,waajiri kutoheshimu sheria za
utumishi kwa kutowatendea haki watumishi kwa kuwapa maslahi yao kwa mujibu wa sheria,sekta
binafsi kuwazuia watumishi kujiunga na vyama vya wafanyakazi na baadhi ya
halmashauri kutoitisha vikao vya mabaraza ya wafanyakazi.
Kinyangoli aliendelea kufafanua kero zinazowasibu
wafanyakazi katika mkoa wa Pwani kwa kutoa shutuma kwa baadhi ya waajiri
kutotimiza ahadi zao kwa wafanyakazi hodari wa mwaka jana kwa kutowapa zawadi
zao hadi sasa na kuomba Uongozi wa mkoa ulifanyie kazi kwa waajiri hao kwani
ahadi zisizotekelezeka kwa wakati huvunja moyo wa utendaji kazi kwa wafanyakazi
wa sekta binafsi na serikali.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,katika hotuba
yake baada ya risala ya wafanyakazi wa mkoa wa Pwani aliwapongeza wafanyakazi
hodari kwa mwaka 2018 kwa utendaji mzuri hata wakaweza kuteuliwa kuwa watumishi
hodari kutoka katika taasisi zao.Aliendelea kulipongeza shirikisho la
wafanyakazi mkoa wa Pwani kwa risala nzuri iliyosheheni mambo mazuri na yenye
tija kwa mstakabari wa utumishi nchini na kusema hakika risala hii imejaa
“Nondo za kutosha”Ndikilo alisema.
Mheshimiwa Ndikilo katika hotuba yake aliahidi kuzifanyia
kazi changamoto zinazo wakabili wafanyakazi ambazo ziko ndani ya uwezo wake na
kwa zile zilizo nje ya uwezo wake aliahidi kuziwasilisha kunakohusika kwa hatua
zaidi. Aliwataka watumishi wa serikali na sekta binafsi kufanya kazi kwa
kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika utumishi sanjari na maadili ya
kazi kwa mujibu wa taaluma walizonazo.Aliwataka wafanyakazi kujiepusha na
matendo ya utovu wa nidhamu katika kazi.”Lazima tuwe na nidhamu ya kazi uvivu
kazini ni sumu katika ajira”Ndikilo alisema.
Aidha Ndikilo alisikitishwa na kitendo cha waajiri wanaotoa
ahadi hewa kwa watumishi hodari na kutowatunuku zawadi zao kwa wakati hili
halikubaliki hata kidogo na kutoa onyo kwa waajiri wanaobagua wananchi katika
ajira hususan watu wenye ulemavu na wanawake na alisisitiza sitakuwa tayari
kufanya kazi na wawekezaji wa aina hii kwani wanafanya vitu vilivyo kinyume na
katiba na sheria za nchi pia.
Mwisho Mkuu wa mkoa aliwataka waajiri kuacha tabia ya kuzuia
watumishi kuhama kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine ni haki ya mtumishi
hivyo kukubali au kukataa uhamisho ni jukumu la wizara ya Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa si suala la mwajiri.”Kama mwajiri toa maoni yako katika barua
ya mtumishi na siyo kumzuia au kukataa kumpitishia barua yake ni kosa mruhusu
na TAMISEMI wataamua”.Ndikilo alisema.