Halmashauri ya Chalinze kwa Mkoa wa Pwani ni halmashauri
ghafi kwa maana kwamba ni kiini cha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo nchini inayotekelezwa kwa kasi.ninaposema ni halmashauri ghafi au
eneo ghafi ni eneo lenye madini mbalimbali ya ujenzi kama mchanga,mawe,kokoto
na mawe mbalimbali yanayotumika kutengeneza vigae katika viwanda vyetu hapa
nchini.
Kwa upande wa kokoto inayopatikana Chalinze ni kokoto bora
katika Afrika Mashariki inayotumika katika ujenzi wa reli ya kisasa yaani “Standard
Gauge Railway”kokoto hii ni kokoto inayokubalika kimataifa ni kokoto ambayo
inatumika katika ujenzi wa reli hii ambayo ni mradi wa kitaifa ambao kimsingi
serikali ya awamu ya tano inautekeleza kwa kasi ya hali ya juu,hivyo
utekelezaji wa mradi huu hatuwezi kusema tunatekeleza pasipo kuitaja Chalinze.
Aidha tuna mradi mwingine ambao umekwisha kamilika katika
jiji la Dar es salaam,mradi wa daraja la juu yaani “Flyover”mradi huu umejengwa
kwa kutumia kokoto inayotoka Chalinze kuanzia mwanzo wa ujenzi hadi mwisho,kwa
hiyo bado wanachalinze na Pwani kwa ujumla tutaendelea kujivunia Chalinze kama
eneo ghafi lenye fursa za kutosha katika kukuza uchumi wa Tanzania kupitia
matumizi sahihi ya mali ghafi inayopatikana Chalinze.
Kokoto ya Chalinze ni kokoto bora inayotumika katika ujenzi
wa miradi mbalimbali ya serikali na ya ile sekta binafsi kwa maana ya ujenzi wa
nyumba binafsi,majengo ya umma,barabara na madaraja mbalimbali katika kuboresha
miundombinu ya barabara nchini.
Serikali iko katika maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa
kufua umeme wa maji katika bonde la mto Rufiji,mradi ambao utaondoa kero ya
upungufu wa umeme nchini.Katika ujenzi wa mradi huu kokoto itakayotumika ni
kokoto kutoka Chalinze,kiasi kikubwa cha kokoto kitatumika katika utekelezaji
wa mradi huu.
Hivyo dhana ya Chalinze kuwa Eneo Ghafi la utekelezaji wa
ujenzi wa miradi mbalimbali ya kitaifa itaendelea kuishi siku zote na
tutaendelea kusema” Chalinze Eneo
Ghafi,Chalinze kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Ujenzi kitaifa”