Tuesday, November 7, 2017

JE UNAFAHAMU KUHUSU SHERIA ZA JINAI?


Sheria za jinai ni sheria zinazoshughulikia makosa ya jinai. Makosa ya jinai Ni makosa ambayo MTU anayafanya dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maantiki hapa Ni kwamba SERIKALI ndiyo yenye jukumu la kulinda wananchi wake na Mali zao,kwa hiyo chochote utakachofanya kuhatarisha Usalama wa wananchi hao au Mali zao ni sawa na kuifanyia kosa hilo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ndiyo maana SERIKALI inabeba jukumu la kumchukulia hatua za kisheria MTU yeyote ambaye atafanya makosa hayo ya jinai. Makosa haya ni pamoja na wizi,kujeruhi,kuvunja ,kuvamia Ardhi ya MTU bila ruhusa yake ,lugha za matusi,kukashifu dini ya MTU yeyote,kutumia madawa ya kulevya,kukutwa na nyaraka za SERIKALI,ulaghai,ubakaji,kughushi,kufanya chochote bila kibali kinachotambuliwa kisheria na mengineyo.
Makosa haya yanaongozwa na sheria ya kanuni ya Adhabu( The penal code), Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(The Criminal Procedure Act),Sheria ya Ushahidi(The Evidence Act) na sheria nyinginezo.
SHERIA YA KANUNI YA ADHABU(THE PENAL CODE CAP 16. R.E 2002)
Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 Ni sheria ambayo inaeleza makosa mbalimbali ya jinai pamoja na adhabu zake ikiwemo makosa yanayohusiana na uhaini,makosa ya uvunjifu wa amani,matumizi mabaya ya ofisi,makosa dhidi ya shughuli za kidini,makosa yaliyo kinyume na maadili,makosa dhidi ya ndoa,mauaji,makosa ya kuhatarisha Afya,uzembe,kujeruhi,wizi,kughushi,makosa dhidi ya utu wa MTU na mengineyo.
Sheria ya kanuni ya adhabu imegawanyika katika sehemu kuu 2 zenye sura 46 na jumla ya vifungu 390 vinavyoeleza mambo mbalimbali yahusuyo makosa ya jinai. Katika sehemu ya kwanza kuna sura 1-5 inayozungumzia kanuni mbalimbali katika makosa ya jinai na sehemu ya Pili kuna sura 6-46 inayozungumzia makosa yenyewe ya jinai na adhabu zake.
Katika sehemu ya kwanza; sura ya I( kifungu cha 1-3) inaeleza juu ya utangulizi. Sura ya II( kifungu cha 4-5) inaeleza juu ya tafsiri za maneno mbalimbali. Sura ya III( kifungu cha 6_7) inaeleza juu ya miaka ya utendaji kazi wa sheria. Sura ya IV(kifungu cha 8-21) inaeleza juu ya kanuni za uwajibikaji katika makosa ya Jinai. Sura ya V(kifungu cha 22-24) inaeleza juu ya wahusika wa makosa ya jinai. Nitaendelea kutoa ufafanuzi wakati mwingine. Mungu awabariki.