Tuesday, March 20, 2018

Mafunzo ya Uandishi wa Tovuti yafunguliwa rasmi Iringa

Mafunzo ya uandishi wa tovuti yamezinduliwa rasmi leo katika manispaa ya Iringa kwa maafisa habari na Tehama kutoka mikoa ya Iringa ,Njombe,Singida,na Pwani.Mafunzo hayo yamefunguliwa leo na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano serikalini ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Rebecca Kwandu. Katika hotuba yake ya ufunguzi  aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini na utayari katika kujifunza kwani taaluma ya uandishi ni taaluma kama taaluma zingine. Hivyo mafunzo haya tunataka yakazae matunda kwa washiriki ili waweze kuisemea serikali kwa umakini kama maagizo Waziri wa TAMISEMI Mhe Jafo alivyotoa maagizo kwenye kikao kazi cha maafisa habari wa serikali kilichofanyika jijini Arusha hivi karibuni.Katika mafunzo haya ya uandishi wa tovuti ni utekelezaji wa vitendo kwa maagizo ya serikali ya kuwataka maafisa habari wawe wasemaji wa taasisi zao kwa kuujuza umma yanayotekelezwa na serikali kupitia tovuti za halmashauri na mikoa Kwandu alisistiza.
Kwa upande wake Mkuu wa mawasiliano wa Shirika lisilo la kiserikali USAID/Tanzania linaloshughulikia Uimarishaji wa mifumo ya ya Sekta za Umma(PS3) Bi Leah Mwainyekule amewataka washiriki kujifunza kwa vitendo ili watakapomaliza mafunzo haya tovuti zikawe hai na watanzania wakapate habari za masuala mbalimbali yanayofanywa na serikali sanjari na elimu kwa umma kupitia tovuti.
Mafunzo haya yanafanyika muda muafaka kwani ni siku tatu zimepita tangu kufungwa kwa kikaokazi cha maafisa habari wa serikali pale alipoagiza Mhe Jafo maafisa habari waisemee serikali kwani ni miradi mingi inatekelezwa na serikali ya awamu ya tano lakini wananchi hawajui kinacho endelea. Kikao kazi hiki kitafanyika kwa siku nne na baada ya hapa mafunzo haya yatafanyika kwa maafisa habari wa mikoa ya Mbeya,Katavi,Songwe,Rukwa,Ruvuma,Lindi na Mtwara.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Rebecca Kwandu akifungua Mafunzo ya Maafisa Habari(aliyesimama)