HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU
TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA
Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Kishapu
anawatangazia wananchi Raia wa Tanzania wenye sifa ya kuomba nafasi za kazi za
mkataba kama ifuatavyo:-
1. Msaidizi wa Hesabu ( Accounts
Assistant ) – Nafasi 4
i.
Sifa za Mwombaji
-
Elimu
ya Kidato cha nne
-
Wenye
cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA.
ii.
Majukumu/Kazi atakazokuwa anafanya
-
Kuandika
na kutunza “Register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
-
Kuandika
hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
-
Kutunza
majalada ya Kumbukumbu ya hesabu.
-
Kupeleka
nyaraka/barua za Uhasibu Bank.
-
kufanya
usuluhisho wa masurufu, karadha, hesabu za banki na Amana.
iii.
Ngazi
ya Mshahara
-
mwombaji
atayaebahatika kuajiriwa kwa mkataba ataanza na Mkataba wa malipo ya Tshs.
390,000 kwa mwezi ngazi ya TGS B
iv.
Masharti ya jumla ya muombaji kazi ya
Mkataba.
-
Awe
Raia wa Tanzania.
-
Awe
na miaka 18-45.
-
Awe
hajawahi kufukuzwa kazi, kupunguzwa, kuachishwa au kustaafishwa kazi katika
Utumishi wa Umma.
-
Awe
tayari kufanya kazi kituo chochote cha Afya ndani ya Wilaya ya Kishapu.
-
Mkataba
utakuwa ni wa mwaka mmoja mmoja kwa kipindi chote cha mfadhili na Mkataba
utarudiwa kulingana na utendaji kazi na maadili ya mtumishi.
-
Kipindi
cha mfadhili kikikoma mtumishi hataingizwa moja kwa moja kwenye Ajira za
Serikali.
-
Waombaji
waambatishe vivuli vya vyeti vya Shule, Taaluma, Kuzaliwa na vitambulisho vya
Taifa kwa wale walioandikishwa.
-
Kila
mwombaji aambatishe na picha ndogo 2 passport size zilizopigwa hivi karibuni.
-
Siku
ya usaili kila mwombaji afike na vyeti halisi vya shule, Taaluma, kuzaliwa na
kitambulisho.
-
Kila
mwombaji aandike kwa ushihi anwani yake na namba ya simu inayopatikana muda
wote kwa ajili ya mawasiliano.
-
Mwisho
wa kupokea maombi ni tarehe 27/07/2017
-
Maombi
yote yaandikwe kwa mkono bila kuchapwa.
-
Maombi
yote yawasilishwe kwa anwani ifuatayo:-
Mkurugenzi
Mtendaji (W)
S.L.P
1288
KISHAPU
NB: Masharti yaliyoainishwa kwenye Tangazo hili yasomwe kwa makini na yazingatiwe
Stephen M. Magoiga
Mkurugenzi Mtendaji (W)
KISHAPU
Nakala:
1.
Katibu
Tawala (M) – Kwa taarifa
2.
Mkuu
wa Wilaya
3.
Waheshimiwa
Madiwani – Watangazieni wananchi
4.
Watendaji
Kata Wote – Tangazeni mbao za Matangazo
5.
Mbao
za Matangazo zote Halmashauri ya Wilaya Kishapu.