Thursday, July 20, 2017

Matatizo yanayotukabili katika Jamii


Kuna msemo wa kilatini unasema; ignoracia juris,non excusat wenye maana kwa kiingereza; ignorance of law is not an excuse  na kwa kiswahili twasema kutokujua sheria sio utetezi au kutojua sheria haiwezi kuwa kinga ya kukufanya usichukuliwe hatua za kisheria kama umetenda kosa lolote kwa mujibu wa sheria hiyo.
Hii ina maana kwamba huwezi kwenda Mahakamani au sehemu nyingine yoyote na kusema nilikuwa sijui kama kuna sheria ya namna hii au nilikuwa sijui kama kufanya kitendo cha namna hii ni kosa kisheria. Hivyo itampa mpinzani wako mwanya wa kuutumia kukushinda na inaweza kukugharimu kupoteza haki zako au kufungwa jela hata kama ulikuwa  na haki tangu mwanzo.
Kumekuwepo na matatizo mbalimbali katika maofisi,familia,kampuni,biashara na kazi. Matatizo hayo ni kudhulumiwa,kunyang' anywa viwanja au Nyumba,kushushwa cheo,kuvunjwa kwa mikataba,kutelekezwa kwa familia,ndoa kuvunjika,wajane na yatima kunyanyaswa,wanafunzi kuacha au kuachishwa Shule,watu kujeruhiwa au kuuwawa,wanasiasa kunyanyaswa au kuteswa na kufungwa jela,wanawake na watoto kubakwa,ukeketaji,wagonjwa wa ukimwi kunyanyaswa kazini,mabinti kulazimishwa kuolewa,wachungaji,mashehe,maimamu,mapadri ña maaskofu kutotendewa haki,waandishi wa habari kujeruhiwa na kufungwa,wazawa kunyanyaswa na wageni mahali pa kazi,wazawa kunyang' anywa Ardhi na wawekezaji na mengine mengi
Ukiyatazama vizuri haya matatizo yote na kuhoji vyanzo vyake na mahali yanapotokea utagundua kwamba asilimia kubwa ya watu wanaotendewa vitendo hivyo hawajui sheria na hawajui waende ili wapate haki zao. Wakati mwingine hata wale wanaowatendea watu hao viteñdo hivyo utakuta hawajui sheria pia isipokuwa wana misimamo ya binafsini. Hata kama wanajua lakini wanatumia mwanya huo kuwatendea
Isivyo halali wengine.
Kwa mujibu wa Maelezo hapo juu,Elimu ya sheria ni muhimu sana kwa kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Upo msemo wa kiswahili usemao;" kama unaona Elimu ni ghali basi jaribu ujinga"Lakini ukweli halisi utaendelea kubaki palepale kwamba;" ujinga ni ghali zaidi kuliko Elimu"
Unaweza pia ukakosa haki zako kwa sababu tu huelewi unatakiwa uende wapi au ukamuone nani na katika muda gani ili uweze kupatiwa haki zako. Tatizo hapa linakuwa sio upatikanaji wa haki,bali ni wewe ambaye ndiye mhusika wa kupatiwa haki hiyo huna ufahamu au uelewa wa kutosha juu ya namna gani unaweza ukaipata. Unaweza pia ukakuta kwamba kama haki hiyo S inapatikana tu ndani ya muda au kipindi Fulani,basi kipindi hicho kinaweza kikapita pasipo wewe kuchukua hatua yoyote na ukajikuta umeipoteza haki hiyo.
 ** _ *Na John Mlyambate
Mwanafunzi wa Sheria*_**